Lady Jaydee Habari Ya Mjini Lyrics, Rama Dee Habari Ya Mjini Lyrics

Zile zama za kugombana
Kuzozana paruana
Zimepita tumeshibana
Jifunza sameheana
Kwa ma ex nimejifunza
Kuwa single si adhama
Na kupenda sioni kosa
Na surrender sina namna

Ninayo dhamana
Kukuhadithia
Lolote linalotibu mmh
Pia ninayo karama
Nishakuangalia
Ni wewe ulie karibu uuuh

Sina haya na penzi lako
Asubuhi adhuhuri
Penzi lifunike na kawa
Nzi wasije ndani

Sina baya na penzi lako
Hata ije tufani
Pwani tufike hata na ngalawa
Dhoruba hatuioni

Wewe ni habari
Habari ya mjini
Wewe ni kibali
Kibali changu mimi

Wewe ndio fahari
Fahari yangu mimi
We mali halali
Mali ya kwangu mimi

Wewe ni habari
Habari ya mjini
Wewe ni kibali
Kibali changu mimi

Wewe ndio fahari
Fahari yangu mimi
We mali halali
Mali ya kwangu mimi

Penye zuri
Baya haliwezi kupenya
Kama moshi
Wa ubani unavyopotea
Hadhi yako zaidi wa muhatibu
Kwa maneno yalivyopangwa
Kugombana ni kawaida
Ukubwa kusameheana

Wangu kinanda, unanipatia
Hisia mwanana unaniletea
Huna matata unaniwezea
Penzi shatashata eeeh
Unanipatia

Sina haya na penzi lako
Asubuhi adhuhuri
Penzi lifunike na kawa
Nzi wasije ndani

Sina baya na penzi lako
Hata ije tufani
Pwani tufike hata na ngalawa
Dhoruba hatuioni

Wewe ni habari
Habari ya mjini
Wewe ni kibali
Kibali changu mimi

Wewe ndio fahari
Fahari yangu mimi
We mali halali
Mali ya kwangu mimi