Nandy – Umenifaa Lyrics

Nandy Wanibariki EP Lyrics
Nandy – Wanibariki EP Lyrics

Umenifaa Lyrics by Nandy

(Wanene)
Wakati wa shida, wakati wa shida
Huniepusha huniepusha mimi

Ni wewe ulinipa njia pasipo kuwa na njia
Ni wewe ulinipa chakula wakati wa njaa kali
Ni wewe ulinifuta machozi wakati wa huzuni
Ni wewe Baba aah

Ina mengi dunia na ina siri nzito
Hata magumu yalipotokea hukuniacha mwenyewe
Kwenye sufuri umenitoa fedheha na laana umeziondoa
Furaha na faraja imenijia Yesu

Umenifaa, umenijaa, wakati wa shida
Umenifaa, wakati wa shida
Umejibu maombi yangu, wakati wa shida
Umenifaa, wakati wa shida

Umetarafu na matendo ya wanadamu
Kwa neno la midomo yako
Umeniepusha na njia za wenye jeuri
Nyayo zangu zi kwako

Nitatengeneza nawe
Nitajiimarisha nawe
Kwa kinywa changu nitakiri
Ulivyo uaminifu wako

Ina mengi dunia na ina siri nzito
Hata magumu yalipotokea hukuniacha mwenyewe
Kwenye sufuri umenitoa fedheha na laana umeziondoa
Furaha na faraja imenijia Yesu

Umenifaa, umenijaa, wakati wa shida
Umenifaa, wakati wa shida
Umejibu maombi yangu, wakati wa shida
Umenifaa, wakati wa shida

Nipokee vumbi nifute
Nishike nisiaibika
Nipokee vumbi nifute
Nishike nisiaibika

Wakati wa shida, wakati wa shida
(Umeniepusha na mengi)
Wakati wa shida, wakati wa shida
Wakati wa shida, wakati wa shida
(Yesu unisaidie)

Written by; Nandy
Released date; 6 March, 2021
Album/EP; Wanibariki

 

Nandy Umenifaa Lyrics